Kwa mujibu wa ripoti ya Idara ya tarjama ya Shirika la Habari la Hawza, nchini Sudan kuna makundi mawili yanayopigana katika vita vya ndani: RSF (Vikosi vya Msaada wa Haraka) na ASF (Jeshi la Wananchi wa Sudan). Kundi la kwanza, ambalo linasemekana linapata msaada wa kifedha na wa vyombo vya habari kutoka katika moja ya nchi za Kiarabu, limejihusisha na mauaji ya raia na ukatili mwingi, kiasi cha kuwasababisha watu milioni 13 kukimbia makazi yao.
Video mbalimbali za kundi la kigaidi la Vikosi vya Msaada wa Haraka zikionesha utekelezaji wa hukumu za kifo na mauaji ya halaiki zimeenezwa kupitia vyombo vya habari. Wakati huohuo, picha za setilaiti pia zimechapishwa zikionesha madoa makubwa na endelevu ya damu ardhini nchini Sudan. Hayo yalikuwa ndiyo aliyoyataja Nathaniel Raymond wa Maabara ya Utafiti ya Chuo Kikuu cha Yale kuwa ni “mauaji ya halaiki ya kiwango cha Rwanda.”
Kwa upande mwingine, tunaona vyombo vya habari vya Kizayuni vya Israeli vikiwahamasisha watu juu ya mauaji haya ya kikatili nchini Sudan, vikidai kwamba badala ya kufanya maandamano na misururu ya maandamano ya kuunga mkono Palestina, watu wanapaswa kuiunga mkono Sudan. Hata hivyo, ukweli ulio wazi ni kwamba mauaji ya Sudan nayo yanatokea chini ya usimamizi wa Israel. Utawala huo wa kidhalimu na wenye kiu ya damu unalifadhili kundi la kigaidi la Vikosi vya Msaada wa Haraka na kulipa mipango ya utekelezaji ya mauaji mabaya dhidi ya wanawake na watoto.
Chanzo: Imenukuliwa kutoka Middle East Eye
Maoni yako